Call me Founder tz
Mwenzenu mi nataka nidabu na Rayvanny uuh niuze sura
Pengine nitukane wasani wa hapa kwetu kama yule Junda
Kajala Paula niwapende pengine labda inaweza ikasaidia
Marapa wote niwachambe, ama niseme yule Lunya wanaibia
Maana sijui ntatoboa vipi
Ama niseme namzidi yule Avril
Yaani yanisumbua
Mawazo kichwani kutwa nawazua, Oooh
Izi kundi kundi zinaboa
Nlikuwaga na ya kwangu ila sikutoboa
Ama niseme natoka na Zuela kuja kuangalia hatuendani. Mmmh
Braza Loki nifanyeje, ama nimtusi Marlow hadharani
Nkiangalia hio ngao za juu najikuta tu mi natamani
Nifanye nini sasa, niwe kama wale na mimi
Nitatokaje, mwenzenu ntatokaje
Nitatokaje, I wish ntatokaje
Nitatokaje, mwenzenu ntatokaje
Nitatokaje, I wish ntatokaje
Kuna muda nawazua, niforce bifu na nani
Pengine itanitoa, nionekane mtaani
Nataka niwe na brand kama Mondi
Kesho nami natambe, nimiliki manoti nijinadi, brandi kwangu iwe genge
Hasa nifanye lipi nitoboe, niwe kama Konde au Vanny boy
Ama nitangaze ndo waaminiooe, hio haiwezekani
Mwenzeni mimi nawaza wohwoh
Nshazunguka kila kona mi youuh
Nimtukane Folo nimchafu, ama niingilie mambo hayanihusu
Ama niposti picha za utupu, naona yote sio poa
Ama niseme natoka na Zuela kuja kuangalia hatuendani. Mmmh
Speki piti nifanyeje, ama nimtusi Nyago hadharani
Nkiangalia hio ngao za juu najikuta tu mi natamani
Nifanye nini sasa, niwe kama wale na mimi
Nitatokaje, mwenzenu ntatokaje
Nitatokaje, I wish ntatokaje
Nitatokaje, mwenzenu ntatokaje
Nitatokaje, I wish ntatokaje