Elige una pista para reproducir
Kila siku zinavyoendelea nazidi tambua
Kumbe adui wa mtu ni wa karibu mno
Kila siku zisongeavyo nazidi tambua
Kumbe adui wa mtu ni wa karibu mno
Awezaye kujeruhi moyo, awezaye kukutesa
Hatoki mbali, ni wa karibu mno
Awezaye kukuumiza moyo, awezaye kukuwekea jeraha
Hatoki mbali, ni wa karibu mno
Nilipoumizwa na mtu wa karibu sana
Nikasema basi ni nani wa karibu na mimi
Katika kufikiri hayo
Nikajua Mungu pekee yake ni wa karibu kwangu
Nikajua kumbe wengi wameumizwa na watu wa karibu
Nikatiwa nguvu ya kuendelea
Tunapomsoma Yesu kwamba alisalitiwa
Aliyemsaliti ni wa karibu mno
Tunapomsoma Habili kwamba aliuwaua
Aliyemuua ni wa karibu mno
Tunapomsoma Yusufu aliuzwa utumwani
Waliomuuza ni wa karibu mno
Ndipo nikasema kumbe rafiki wa karibu ni Mungu tu
Kanga Mkuu maishani mwangu
Njoo Yesu, njoo (njoo Yesu, njoo)
Umebaki mwenyewe (pekee yako watosha)
Njoo Yesu, njoo (njoo kwetu, Baba)
Utugange mioyo (mioyo imeinama)
Njoo Yesu, njoo (wanadamu wametujeruhi)
Umebaki mwenyewe (umebaki mwenyewe)
Njoo Yesu, njoo (wewe tu, Baba)
Utugange mioyo
Unaposikia mjane kadhulumiwa kila kitu
Aliyemdhulumu ni wa karibu mno
Unaposikia yatima kanyang'anywa kila kitu
Aliomnyang'anya ni wa karibu mno
Wengi wamelizwa na watu wa karibu mno
Umebaki mwenyewe Mungu
Kila mtu na msiba wake mwenyewe, mm
Karibu kwetu wewe Mungu, rafiki wa karibu
Nilipojua mwanadamu tofauti na wewe Mungu
Nikasema watosha wewe tu
Wanadamu tunageukana, tunatendeana
Asingekuwepo Mungu tungeshamalizana wote
Sina njema kwa mwanadamu, kila nifanyalo nakosea
Wewe tu Baba unanipenda kweli
Mwandamu amekaa kutafuta baya kwa mtu
Usiyetafuta baya kwangu, Baba, Baba, wewe
Maisha haya ni Mungu umetupa
Kwako tunajiweka tuwe salama
Mioyo ya wengi inalia, Baba
Amejeruhiwa na watu wa karibu mno
Karibu ndani yetu ugange majeraha
Umebaki mwenyewe tu
Mjane ametendwa, yatima ametendwa
Umebaki wewe tu, wewe tu, Baba
Faraja ya wengi, mwokozi wa wengi
Tuokoe, Baba, katikati ya adui
Mganga mkuu, tibabu mwema wewe
Ganga mioyo yetu, imejeruhiwa
Nilitendwa na ndugu, nilachwa na ndugu
Ukasimama wewe, Baba, mm
Nikasema, "Yesu, njoo"
Nikasema, "Njoo, Yesu, njoo"
"Njoo, Yesu, njoo kwangu, njoo"
Njoo Yesu, njoo
Umebaki mwenyewe (umebaki mwenyewe, Baba)
Njoo Yesu, njoo (njoo kwetu, Baba)
Utugange mioyo (sisi tumechoka mno)
Njoo Yesu, njoo (tutie nguvu tena)
Umebaki mwenyewe (umebaki wewe, Baba)
Njoo Yesu, njoo (kwetu njoo)
Utugange mioyo (wanadamu tunatendana)
Njoo Yesu, njoo (wewe tu, watupenda kweli)
Umebaki mwenyewe (umebaki wewe, Baba)
Njoo Yesu, njoo (njoo, Baba, njoo)
Utugange mioyo
Njoo Yesu, njoo (njoo, Baba, njoo)
Umebaki mwenyewe (rafiki mwema)
Njoo Yesu, njoo (njoo, Baba, njoo)
Utugange mioyo (Baba wa mayatima)
Njoo Yesu, njoo (umeoa wajane)
Umebaki mwenyewe (ganga mioyo yetu)
Njoo Yesu, njoo (njoo Yesu, njoo)
Utugange mioyo (njoo, Baba, njoo)
Njoo Yesu, njoo (njoo, Baba, njoo, Baba)
Umebaki mwenyewe (uwe nasi, Baba)
Njoo Yesu, njoo (njoo, Baba, njoo)
Utugange mioyo (wenyewe tumeshindwa)
Njoo Yesu, njoo (wenyewe tumeshindwa)
Umebaki mwenyewe (rafiki mwema)
Njoo Yesu, njoo (njoo, Baba, njoo)
Utugange mioyo (Baba wa wasio na baba)
Njoo Yesu, njoo (mume wa wasio na mume)
Umebaki mwenyewe (wewe Baba)
Njoo Yesu, njoo (Baba Baba, Baba)
Utugange mioyo