Elige una pista para reproducir
Nilidhani maumivu huisha
Lakini mwaka umekatika
Naomba uniulizie
Kama mbinguni wanaruhusu
Nije nikutembelee
My baby, my sweetie
Hivi na mimi unanimisi kweli?
Huko uliko najua siwezi kufika
Ila natamani nikutembelee...
Najitumisha message WhatsApp
Jana nimebadilisha dp yako ya insta
Najidanganya pengine umesafiri
Junior anauliza bado utarudi lini.
Oh baby, natamani nikufate
Siuwezi huu upweke
Kila nikilala machozi yanatoka yenyewe
Naumia....
Nilidhani maumivu huisha
Lakini mwaka umekatika
Naomba uniulizie
Kama mbinguni wanaruhusu
Nije nikutembelee
Bado ndoto zinanijia
Siku niliyokufunika na mchanga
Sijawa sawa tangu siku ile
Kuondoka kwako kumenivunja...
Waulize kama naweza
Kukuletea machungwa
Najua unapenda ndizi, nitakuletea
Naomba uniulizie
Kama mbinguni wanaruhusu
Nije nikutembelee
Oh baby, natamani nikufate
Siuwezi huu upweke
Kila nikilala machozi yanatoka yenyewe
Naumia....
Upweke umenishinda mama...
Umeniachia watoto
Kama unaniskia...
Waulize kama naweza kukutembelea...