Оберіть трек для відтворення
Nita Amini
Verse :
Sasa naapa Hakuna miungu ntaamini
Satajitia unajisi , Chakula cha ufalme
Na Sitauza urithi wa wokovu,
anasa za Kisasa
NiNa uhakika waweza , waweza kuniponya,
Hata usipo niponya Sitaabudu Masanamu
Chorus :
Naelewa maji na moto nitapita
Kwenye uvuli wa mauti
Nina wewe sitaogopa kamwe
Mungu wangu wanishika mkono
Wautuliza moyo wangu,
Si na mashaka wanibeba mgongoni
Waweza tuma neno la uzima,
libadishe yote
Hata usiyafanye hayo yoote
Bado nitaamini
Verse :
Si Mara y’a kwanza
wanitowa katika magumu
Ni na ushuhuda zaidi ya moja
We ni mwaminifu
Ni na historia maalum
We ni chemchemi ya uzima.
Outro :
Nitaamini, bado nitaamini
Ukiniponya nitaamini
Hata usiniponye bado nitaamini
Ukinijibu nitaamini
Hata usinijibu bado nitaamini
Ukibadilisha nitaamini
Hata usibadilishe bado nitaamini
Kwenye uvuli wa mauti bado nitaamini
Nina ushuhuda, wewe ni mwaminifu