Оберіть трек для відтворення
Let me find a reason to believe
In your saving grace just for me
Kukwamini Yesu ni vita
Na sheria zako si rahisi
Maswali yajaza fikira
Mbona mateso na magonjwa mengi
Mbona vilio, machozi hayaishi
Wasema watupenda ni kweli
Na utatupeleka mbinguni
Mahali penye raha na faraja milele
Tusubiri hadi ufike
Na majibu yote utupe
Kwa hivyo nitaamini, na kuweka shaka mbali
Nitatangaza neno, sitanung'unika mimi
Japo kunayo mengi yanayonivuta mbali
Nitachagua yanayonileta kwako
Nitachagua Amani unayonipa
Ntatafuta kote, sababu ya kutoa maisha kwako Bwana
Sitamani mashaka, nipatie upendo ili nikaze mwendo safarini
Safarini
Badala ya chuki nipe upendo
Badala ya ujinga nipe hekima
Badala ya uzembe nipe nguvu zako tele
Nitangaze neno lako tu
Nifanye mapenzi yako tu
Kwa hivyo nitaamini, na kuweka shaka mbali
Nitatangaza neno, sitanung'unika mimi
Japo kunayo mengi yanayonivuta mbali nawe
Nitachagua yanayonileta kwako Yesu
Nitachagua Amani unayonipa
Ntatafuta kote, Sababu ya kutoa maisha kwako Bwana
Sitamani mashaka, nipatie upendo ili nikaze mwendo Safarini
Nikaze mwendo hmm hmm hmmm
Nikaze mwendo hmm hmm hmmm
Nikaze mwendo hmm hmm hmmm
Na hata mambo yawe vipi, najua wewe uko nami
Kila siku, Kila saa, Kila dakika na sekunde
Uko nami safarini, hmm hmm
Uko nami safarini, hmm hmm hmmm